Breaking

Showing posts with label MUSIC. Show all posts
Showing posts with label MUSIC. Show all posts
July 18, 2017

Linah Akana Taarifa za Kujifungua

Msanii Linah Sanga  'Ndege Mnana' amekanusha taarifa zinazoenea mtandaoni kuhusu suala la kujifungua na kuwataka watu wazipuuzie huku akiwasihi mashabiki zake waendeee  kusubiri taarifa iliyo sahihi kutoka kwake na kwenye mitandao yake ya kijamii.

Linah amekanusha taarifa hizo kupitia EATV na kusema kwamba anashangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni huku akiwa hajui mtu anayesambaza taarifa hizo ana malengo gani.

"Hongera ya nini mbona mimi bado mjamzito? Sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo ana malengo gani? Nawaomba mashabiki zangu waniombee kwa sasa hivi nikiwa nakaribia kwenda kujifungua hivi karibuni ingawa siwezi kusema ni lini kwani siyo vizuri, watu wanatakiwa waone. Mungu akinisaidia taarifa watazipata kupitia kwangu mwenyewe au kwenye mitandao yangu ya kijamii," Linah alifunguka .

Katika hatua nyingine Linna ameongeza kwamba sababu ya za kutoonekana sana kipindi cha hivi karibuni hakujasababishwa na kisirani, hivyo kutoonekana kwake zipo sababu ya msingi.

"Ukweli nina sababu zangu za msingi zinazonifanya nisionekane, Ninachomshukuru Mungu kuwa na mimba hakujanifanya niwe kisirani ila baada ya ya sababu zangu kuisha nitaonekana kama kawaida. Niombeeni nijifungue salama", aliongeza

EATV inamuombea mwanamuziki Linah maandalizi mema ya kumpokea mtoto wake wa kwanza.

July 18, 2017

Gigy Money Ataja Sababu iliofanya Apungue Kwa Kasi Mpaka Watu Wanamsema

Video vixer asiyeisha sekeseke mitandaoni kila kukicha, Gigy Money ameamua kuweka wazi sababu iliyopelekea mwili wake kupungua.

Gigy ameeleza kupitia U-Heard ya Clouds Fm kuwa kilichosababisha ni kupungua mwili wake ni kufanya mazoezi iliaweze ili aendane na soko la mavideo queen wa mbele.

“Kuna Gym na dawa zinauzwa mbona huko Instagram, bhana ila mie naenda Gym ndiyo maana nimepungua,” ameeleza Gigy.

Baadhi ya watu mbali mbali katika mitandao ya kijamii hasa Instagram wamekuwa wakihoji na wengine wakimtuhumu mrembo huyo kufulia ndio maana amekuwa akipungua kila kukicha hasa makalio.