Breaking

UMUHIMU WA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO

MITANDAO YA KIJAMII INA NAFASI GANI KATIKA KUKUZA BIASHARA YAKO??

Leo ninapenda tuangalie matumizi ya mitandao ya kijamii ina nafasi gani katika kukuza na kuendeleza biashara yako na kuongeza mauzo/utoaji wa huduma.

Mitandao ya kijamii ama social network kwa lugha jingine, ipo mingi sana baadhi kuna Facebook, Instagaram, Telegram, badoo, WhatsApp na Linked in. Mitandao hii mara nyingi imekuwa ikitumika kama mahali pa kupotezea mda baada ya watu kufanya shughuli zao za kawaida, nataka nikwambie rafiki unayesoma Makala hii kuwa kuna siri kubwa iliyojificha ndani ya mitandao ya kijamii kuusu utajiri na ni watu wachache sana 5% ndio wanafaham siri hiyo ebu jiulize ni kiasi gani cha vocha ambacho unatumia kudowload video ama nyimbo za kawaida je hufikirii upande wa pili kama vocha ile ile ya ash 500 unaweza kuitumia katika kukuza biashara yako. Haya angalia sasa faida ya kutumia mitandao ya kijamii ndani ya biashara yoyote.

1. UWEZO WA KUWAFIKIA WATU WENGI NDANI YA MDA MCHACHE
Nilipoanza biashara ya mtandao ama (Network Marketing )nakumbuka nilikuwa sina pesa kabisa(broke), sikuwa na pesa ya kuandaa semina wala kusafiri ili nikutane na timu yangu ya kibiashara, niliamua kuwekeza katika mitandao ya kijamii, nilijifunza njia mbalimbali za kuweza kuwafikia wateja wangu, pia jinsi gani ntaweza kuwafikia watu wenye uhitaji wa biashara, pia nilianza kuandika Makala ambazo zinahusu maisha yangu ya kiabiashara na pia huduma ambazo nazitoa, siwezi kusema ilikuwa rahisi kwani vijana wengi tumezoea kutumia mitandao hii kwa mambo ya kawaida hivyo mtu kukubali kazi yako hadi akalike na kucoment kwenye post yangu inachukua mda.
Niliamua kuchapisha ukurasa wangu wa facebook (Jina: AMKA)  kutoka kuwa wa kawaida kupost mambo ya siasa na udaku, sasa nikaanza kupost mambo ya kibiashara, nilipata changamoto sana kutoka kwa marafiKi na baadhi ya jamaa zangu, walijua natania nilipoanza lakini niliweza kuwa na mwendelezo kila siku nilipost ujumbe mpya sikujali mawe mangapi yalirushwa kwangu niliangalia mbele kuna asali na maziwa ambayo ni mafanikio yananisubiri. Lakini napenda kukwambia kuwa kama unasoma post hii basi nakupongeza sana maana nawe unaweza ukabadilika ukaungana nami na ukaweza kuleta matokeo chanya kwa watu wanaokuzunguka.

2. KUWAFIKIA WAHUSIKA TU(TARGETED AUDIENCE) KWA URAHISI.
Huwa napenda kuita SNIPER MARKETING vs SHORTGUN MARKETING , hebu tuangalie mfano wa kawaida kati ya mazingira ya watu hawa wawili, mimi Adam nataka nimtumie Aunt yangu aliyepo maeneo ya Posta Dae es salaam  barua ya mwaliko wa harusi lakini sijui nyumba yake, njia ya kwanza nikaamua kukodi helikopta nikaandika barua nyingi ambazo zinafanana kisha nikawa nazirusha maeneo ya posta ili Aunt yangu akiokota mojawapo basi apate ujumbe wangu.

Njia ya pili nikaamua kutafuta anwani yake kisha nikamwandikia barua na nikaituma.
Je rafiki msomaji unapata picha gani katika njia hizi mbili??

Njia ya kwanza (Shortgun Marketing) itanichukua gharama kubwa kukodi helikopta ili kuweza kurusha barua zangu za mwaliko na pia itachukua mda mrefu ili ujumbe uweze kumfikia Aunt yangu.

Njia ya pili ambayo ni (Sniper Marketing) itanigarimu kias kidogo sana cha pesa kwa ajili ya kunua bahasha haitazidi sh 500 pia na pesa ya kulipia utumaji wa barua nayo haiwezi kuzidi sh 5000, na barua yangu itafika kwa wakati.
Sasa jiulize biashara yako unatumia Sniper ama Shortgun Marketing, kama hujui walengwa wa biashara yako nia akina nani basi bado unatumia njia za kizamani, na itachukua muda mrefu kwa wewe kweza kufikia mafanikio, kwa nini nakwambia hivi? DUNIA INABADILIKA SANA teknologia inakua hivi usipokuwa mtafiti na mbunifu utaachwa nyuma.

3. KUTENGENEZA BRAND YAKO NA UKAWA SUMAKU KWA JAMII INAYOKUZUNGUKA.
Jiulize maswali haya kabla hujaendelea kusoma makala hii, hivi utajisikiaje kila siku unaamka asubuhi unakutana na Msg Zaidi ya 50, na Misd Call nyingi za namba mpya na watu hao wote wakihitaji uwafundishe namna gani wanaweza kujiajiri na kuongeza kipato chao
Naamini utajisikia vizuri na huu ndo utakuwa mwanzo wa mafanikio kwako, usifikiri kufanikiwa ni kuwa na pesa nyingi, nataka nikwambie rafiki yangu  kwamba pesa ni kitu kidogo ambacho kinaweza kuisha lakini ukishatengeneza SOCIAL CAPITAL, jinsi gani watu wakakuamini na kukuthamini basi haya ni mafanikio makubwa sana.

Hivo mitandao ya kijamii inakuwezesha kutengeza na kukuza thamani ya jina lako kwa kutumia gharama ndogo sana ya bando la  vocha ya sh 500/1000/= Kumbuka unapotaka kutengeneza Brand yako kubali kulipa gharama { maana yake uwe tayari kutumia mda wako vizuri, uwe tayari kusoma vitabu vya Kibiashara, uwe tayari kupambana na changamoto, uwe tayari kubezwa na kutukanwa na watu ambao wanapenda ubakie chini siku zote/wasio waelewa} na kitu cha muhimu ukubali kutoa thamani yako kwa jamii inayokuzunguka, wape watu huduma na hapo ndipo watu wataweza kukupa faida, kuwa sehemu ya suluhisho la matatizo ya watu ndipo utaweza kutengeza faida.

Kwa mawasiliano
Whatsap/ text  +255685303567
Email: laurentandrea3@gmail.com
Asanteni.

No comments:

Post a Comment