Breaking

Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts
December 31, 2018

Kilichojificha DODOMA KUTOTAJWA KIMAPATO

December 31, 2018 Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amefanya mazungumzo na Waandishi wa habari ofisini kwake Dodoma ambapo ametoa ripoti ya utendaji kazi uliofanyw ana ofisi yake katika kipindi cha mwaka 2018 lakini kubw azaidi ametoa siri ya jiji lake kutajwa kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato nchi nzima. http://bodelen.com/afu.php?zoneid=2265899




July 19, 2017

Mghwira amvaa Lowassa, asema kuhama chama ni ufisadi wa kisiasa

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa njia aliyoitumia aliyekuwa mgombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu uliopita kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ilikuwa ni aina fulani ya ufisadi wa kisiasa.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifanya mahojiano na Gazeti la Mwananchi ambapo amesema kuwa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema njia aliyoitumia ilikuwa ni aina mojawapo ya ufisadi kwakuwa hakupitishwa na chombo chochote ndani ya chama chake.

Amesema kuwa hata katika Kampeni za uchaguzi mkuu, Ukawa haikuzungumzia suala la ufisadi kwakuwa kiongozi huyo teyari alikuwa ameshajiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

“Kwenye Kampeni za mwaka 2015 chama kikuu cha upinzani (Chadema) hakikuwa tena kinazungumzia suala la ufisadi, labda kwa hofu kuwa mshtumiwa wa ufisadi alikuwa mgombea wao, kwa bahati mbaya wao ndio waliibua tuhuma za ufisadi, lakini kuondoka kwa Dkt. Slaa nako kulikuwa ni tatizo, ingawa watu hawakutaka kulifuatilia,” amesema Mghwira.

Aidha, Mghwira amesema kuwa watu walitakiwa kuhoji sababu za kuondoka kwa Dkt. Slaa na alikoelekea, nakuongeza kuwa ni ajabu kwa kiongozi anayepigania demokrasia anaingia kwenye chama na kugombea nafasi ya urais bila kupitishwa chombo chochote.

Hata hivyo, Mghwira ambaye ni kiongozi wa kwanza wa upinzani kushika wadhifa wa ukuu wa mkoa tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, amesema kuwa njia waliyotumia Chadema si tu inarudisha nyuma siasa za upinzani, bali haikutoa picha nzuri ya demokrasia ndani ya upinzani.

Alikerwa kuvuliwa uenyekiti
Katika mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Shanty Town mjini Moshi, Mghwira alikumbuka karaha aliyoipata baada ya furaha ya kuaminiwa na Rais na kupewa wadhifa huo.

Alisema kama si ubabaishaji wa kisiasa Tanzania, asingeondolewa kwenye uenyekiti wa ACT-Wazalendo.

“Changamoto niliyokutana nayo ACT-Wazalendo kama mwenyekiti ni kukosa wigo sahihi wa kisiasa kwa sababu kama tungekuwa tunafanya siasa sahihi, nisingeondolewa uenyekiti,” alisema.

Mghwira alisema, “Naapishwa tu kuwa RC (mkuu wa mkoa) kesho yake naondolewa tena tukiwa tumepanga kukutana kwenye kikao na mpaka leo hatujawahi kukutana.

“Nimesoma kwenye magazeti kuwa mrithi wa Mghwira kutembelea mikoa saba, yaani na mrithi ameshapatikana. Hizo si siasa, huo ni ubabaishaji. Ubabaishaji wa kisiasa Tanzania ni tatizo,” alisema.

Aliongeza, “Sisi kina mama tukisimama imara tunaweza kuondoa dhana hii ya siasa za ubabaishaji. Ni siasa za kipuuzi kabisa. Mmekubaliana mkutane muongee, hamuongei wenzako wanakaa pembeni. Umechaguliwa na mkutano mkuu unaondolewa na kamati ndogo. Watu 370 karibu 400 hivi walikuchagua, siku ya kuondolewa unaondolewa na watu watatu au wawili au mmoja. Hiyo si siasa ni dalili tosha kuwa hakuna siasa.”

Alisema mbaya zaidi ni kuwa watu wanaokuondoa hawakutumwa na mkutano mkuu, wala hawakukaimishwa na kamati kuu.

Hakuna upinzani nchini
Baada ya kujumuisha yote hayo na hasa alivyotimuliwa kwenye uongozi, mkuu huyo wa mkoa akawa na jibu moja kuhusu siasa za upinzani, “Hakuna siasa za upinzani, bali zilizopo ni za kurudishana nyuma maendeleo.

“Siasa ni kitu kizuri kwa maana ya ile mijadala, kubadilishana mawazo na kuzungumzia masuala ya itikadi, mipango ya kijamii... hakuna hiki kitu Tanzania.”

Badala yake alisema, “Tumeweka siasa kama ni uhasama kati ya chama tawala kilichoshinda kihalali na vyama hivi vingine. Kila siku watu wanatafuta makosa ya wenzao (Serikali) hata kama inafanya vizuri. Hiyo sio siasa.

“Vyama vya upinzani hapa hatuendeshi siasa. Awali, chama chochote kitakachoibuka na siasa inayoeleweka kinaweza kutawala nchi hii kwa miaka 100 ilimradi tu kitoke na siasa inayoeleweka.”

Mghwira alisema, “Vikitokea vyama vitatu vinaendesha siasa inayoeleweka tunakuwa mahali pazuri zaidi. Kwa maana kwamba wale wakiongea jambo lao, hata kama hawatawali, mtawala asikie na kuthamini.

“Sisi hapa Tanzania kuna aina ya siasa za kudidimizana. Kwa sisi wanawake wanaharakati tunaziita PhD (pool her down). Unavutwa tu chini hutakiwi kukua. Nchi haiwezi kwenda kwa staili hii.”

Alisisitiza, “Kuna watu wanafikiri kwamba ili kitu kiwe sahihi ni lazima wao wakifanye (upinzani) lakini kikifanywa na watu wengine hakiko sahihi. Hiyo ni kutokuwa mwanasiasa. Kuwa mwanasiasa si kugombana ni kuwa na uwezo wa kujenga hoja, kuitetea na kuisimamia. Mwenzako akija na hoja kubwa zaidi kubali.”

July 19, 2017

DC Amuweka Ndani Dk Mary Nagu (Mbunge wa Hanang -CCM )

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu  jana alishikiliwa kwa muda polisi baada ya kutokea vurugu katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho.

Dk Nagu aliyewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa Serikali za awamu mbili zilizopita, alishikiliwa kwa muda  na kuachiwa baada ya kuhojiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Masawe alisema Dk Nagu alifikishwa kituoni kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye kikao cha kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Hanang baada ya makundi mawili kujitokeza.

Masawe alisema baada ya mahojiano kufanyika na kuandika maelezo, kwa kuwa mgogoro huo ulikuwa ni mambo ya ndani ya CCM walimwachia.

"Taarifa ambazo nimepata ameachiwa baada ya kuandika maelezo na tayari walifikia makubaliano wenyewe," alisema.

Awali, mkuu wa wilaya hiyo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, Sara Msafiri alisema: "Ni kweli amekamatwa lakini nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza.”

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zimeeleza Dk Nagu alikamatwa kutokana na malumbano ya kupitisha wagombea wa uchaguzi ndani ya CCM.

July 18, 2017

Nahisi Mke Wangu Anatembea na Binamu yake....

Mimi ni mwanaume wa Dar kabisa nina kifriji cha bia za ofa na kitimoto na kazi yangu huwa ni upambe kwa matajiri na watoto wa mjini japo nina kiofisi cha kuzuga cha insurance broker na clearing and forwarding kama ilivyo ada yetu wanaume wa Dar.

Sasa balaa linalonikabili ni hivi juzi wife aliniomba aje mtoto wa shangazi yake akae kwangu kwa kuwa alipata fursa ya kujifunza kazi ya ufundi magari gereji ya karibu na nyumbani kwangu. Bila hiyana nikamkubalia, sasa balaa tulipoenda kumpokea Ubungo kushuka kijana bonge la handsome afu mwili wa mazoezi.

Kimsingi wamezoeana sana na wife. Akiamka asubuhi mimi naandaliwa chai sausage na yai yeye anapasha kiporo cha ugali anashushia na mchicha anaoulima bustani hapa kwangu. Baada ya hapo anaenda jogging akirudi ndo anaelekea gereji mayaweee nafwa

Gereji wanatoka saa 8, kuna siku nikarudi ghafla mchana nikakuta amekaa na boxer na singlet miguu bonge la gimbi kifua kimejaa minywele afu anapiga pasi nguo za wife mwee ndifwaaa mwiyenu

Kinachoniudhi anajifanya ana heshima sana kwangu mara anipokee mizigo mara amsindikize wife sokoni aghhhggaaaaa come on shittt.

Sasa juzi kati walitoka na wife kumpeleka sokoni sijui kilinikumba nini nikaingia kupekua chumba chake nikakuta kitenge cha wife kitandani kilichopigwa pasi nikajifariji itakuwa ni hii tabia ya kumpigia pasii cheki kwenye droo nikakuta mafuta ya 'KY Gel' ila hayajatumika kabisa.

Kumuuliza wife naona nitapoteza ushahidi au nitaharibu uchunguzi basi nimekuwa kila wakitoka nakagua yale mafuta, ni wiki sasa hayajafunguliwa.

Jamani watemi nitumie gia gani kumtimua huyu maana nimejikuta narudi saa nane kumhofia jamaa.
.
.
NAOMBENI USHAURI TAFADHALI

July 18, 2017

Je Kuna Ukweli Teuzi za Magufuli ni za Ubaguzi wa Kikanda?

Nimemsikiliza Mh Tundu Lissu jana, mbunge na mwanasheria wa chadema, akilalamika kuwa teuzi za mtukufu Rais ni za kikanda.

Mheshimiwa Lissu alidai kwa kueleza teuzi nyeti za serikali kuwa ni za kibaguzi na hazileti picha ya kitaifa.

Lissu aliwataja watu wafuatao kuwa wanatoka kanda ya ziwa.
1. Mwanasheria mkuu
2. Mkuu wa JWTZ
3.IGP
4.Mkuu wa usalama wa taifa
5.Katibu wa fedha na naibu wake
6. Katibu mkuu

Lakiki Lissu hakuangalia nafasi nyingine nyingi ambazo Rais ameteua watu ambao sio kanda ya ziwa, mfano
1. Baraza la mawaziri, 
2. Wakuu wa mikoa wanatoka kila kanda
3. Waziri mkuu
4. wakuu wa wilaya

Bado hoja ya Lissu inahitaji kujadiliwa ili kuweza kubaini ukweli wa jambo hili vinginenvyo etaleta sinto faham nyingi sana kiasi cha watu kushangaa mbona Rais hazindui miradi katika mikoa ya kaskazini.

Hatuwezi kuacha hili jambo kuelea, nilazima Lissu ajibiwe kwa ushahidi aondoe hii dhana potofu.

General Mangi/Jamii Forums

July 14, 2017

Hajawahi Kujamiiana, na Bado Ananibania Mpaka Sasa

Habari Wadau... Nina mpenzi wangu, nampenda saana, we have been dating for 1 year and 9 months now. Hatujawahi ku-doo. At the early stages of our relationship, i once cheated, na nlimuumiza sana, lkn nilikiri makosa, na akanisamehe, and we trust each other once again, na tunaendelea vzri sana kwakweli, mapenzi yapo vizuri.

The issue is, she is a virgin,ive proved it, coz sometimes tunakua faragha pamoja, we kiss and romance, bt we dont do it,, lakini kila nikimuomba, ananiambia she is not ready, she told me to wait for another year, i am ready to wait bcause of the love i have for her, lkn maswali hayaishi kichwani mwangu, je, nikiendelea kungoja, mpaka muda huo, which will b almost three years, will it b not too long? Hatakuja kunidharau na kuniacha njia panda? Will she keep on loving me? Am i doing the right thing kungoja,?? Samtymz nakua na hamu and i dont want to cheat on her,, na maswali mengine mengi,, nishaurini wadau? Am i going in the ryt track? Should i wait?? Au nimuombeje akubali na ajue kua kwa muda wote niliokua nae, kama ningekua nahitaji ngono tu, ningeshamuacha, im rreally into her, na akiendelea kua na tabia njema, Mungu akipenda tutaoana,kwasababu sijaona baya lolote kwake,, ushauri wadau. Shukrani sana