Nimemsikiliza Mh Tundu Lissu jana, mbunge na mwanasheria wa chadema, akilalamika kuwa teuzi za mtukufu Rais ni za kikanda.
Mheshimiwa Lissu alidai kwa kueleza teuzi nyeti za serikali kuwa ni za kibaguzi na hazileti picha ya kitaifa.
Lissu aliwataja watu wafuatao kuwa wanatoka kanda ya ziwa.
1. Mwanasheria mkuu
2. Mkuu wa JWTZ
3.IGP
4.Mkuu wa usalama wa taifa
5.Katibu wa fedha na naibu wake
6. Katibu mkuu
Lakiki Lissu hakuangalia nafasi nyingine nyingi ambazo Rais ameteua watu ambao sio kanda ya ziwa, mfano
1. Baraza la mawaziri,
2. Wakuu wa mikoa wanatoka kila kanda
3. Waziri mkuu
4. wakuu wa wilaya
Bado hoja ya Lissu inahitaji kujadiliwa ili kuweza kubaini ukweli wa jambo hili vinginenvyo etaleta sinto faham nyingi sana kiasi cha watu kushangaa mbona Rais hazindui miradi katika mikoa ya kaskazini.
Hatuwezi kuacha hili jambo kuelea, nilazima Lissu ajibiwe kwa ushahidi aondoe hii dhana potofu.
No comments:
Post a Comment