Breaking

Showing posts with label HABARI..... Show all posts
Showing posts with label HABARI..... Show all posts
July 18, 2017

Polisi Dar watia Mbaroni Madalali Bandia 12 Wanaojihusisha na Wizi wa Shehena za Bidhaa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini dsm linawashikilia madalali bandia 12 wanaodaiwa kuendesha vitendo vya wizi wa shehena za bidhaa za mamilion ya fedha huku wakitumia malori yaliyowekwa namba bandia pamoja na nyaraka bandia ili kufanikisha wizi huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Giles Mroto akizungumza na wanahabari amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kupata taarifa ya malori ya bidhaa za vifaa vya ujenzi na ngano vyenye thamani ya shilini milion 400 , ambayo yalichepushwa na watuhumiwa badala ya kupelekwa geita yalipelekwa mbeya na kufichwa.

Amesema watuhumiwa hao pia walibainika kuwa na mihuri,nyaraka bandia mbalimbali za ukaguzi wa mizigo lakini pia redio call ambapo baadhi yao walijifanya maafisa wa polisi katika kufanikisha wizi huo.

Aidha kutokana na kukithiri kwa wizi huo Kamanda mroto ametoa wito kwa wale wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi kwa kuwatumia madali au mawakala kuwa waangalifu.

Chanzo: Channel 10

July 14, 2017

RC Gambo ameonya shule kugeuzwa kuwa matawi ya siasa

Mkuu wa mkoa wa ARUSHA,MRISHO GAMBO,ameonya shule kutogeuzwa kuwa matawi ya siasa na walimu wakuu kuacha kuruhusu hali hiyo na iwapo watabainika kukiuka agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.

Gambo anatoa onyo hilo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakuu wa shule za sekondari ARUSHA-TAHOSA-na kutoa angalizo kuwa shule ni eneo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi na si kitovu cha siasa.

Amesema kuna tabia imeanza kuibuka ya baadhi ya shule kugeuzwa vijiwe vya siasa na kuyataka mashirika yasiyo ya kiserikali endapo yanalengo la kusadia wanafunzi wanaopata mimba mashuleni ni vyema wakaweka mawakili wakuwaadhibu watu wanaowapa ujauzito wanafunzi.

Wakuu hao wa shule wametaja kuwa mkutano huo kuwa ni mojawapo ya jitihada mbalimbali wanazozifanya kuboresha elimu katika shule za sekondari mkoani ARUSHA.