Msanii wa Bongo Fleva, Timbulo amedai yeye anampenda mwanamke yeyote ila kuna wakati unafika anachanganyikiwa katika kuchagua.
Muimbaji huyo ameeleza kuchanganyikiwa huko kunakuja pale anapompenda wanamke mweusi lakini anapomuona mwanamke mweupe anakuwa anavutiwa nae zaidi.
“Nikawa najiuliza hii inakuaje haya nasema napenda mwanamke vimodo lakini nikiona mwanamke mwenye umbo kubwa nachanganyikiwa, baadaye nikaja kugundua mimi mjinga moyo wangu unanidanganya, kumbe natakiwa kupenda kile ambacho kitakuwepo kwa wakati uliopo,” amesema Timbulo.
Ameongeza, “Kwa hiyo mimi sijawahi kuwa na ‘choice’ kwamba napenda mwanamke wa hivi au hivi inategema na wakati tu siku zingine napenda mweusi, mweupe, mwembamba au unene” amesisitizaTimbulo
No comments:
Post a Comment