Mwalimu wa somo la kiingereza toka china-Ma Yun a.k.a Jack Ma, Episode ya pili [2]
Baada ya kuomba nafasi za kujiunga na masomo ya elimu ya juu Zaidi ya mara tatu na kushindwa zote ,Professor Yu alimuambia Jack Ma, kuwa uwezo wako wa kufaulu somo la hesabu ni mdogo sana,kama ikitokea umefanya vyema somo la hisabati ,naahidi kuandika jina langu kinyume nyume.
Kauli hii ilimuumiza sana Jack Ma ,na alikuwa na njaa ya kusomea ualimu katika chuo cha, Hangzhou Teacher's Institute ,Kuna msemo unaosema,’’Nuru iliyopo kwenye macho yako inatokana na hazina ya malengo na njaa iliyopo kwenye moyo wako’’ huu ni msemo uliompa Jack Ma njaa ya kufikia kilele cha mafanikio yake.
Alitengeneza utaratibu wa kukariri formula zote za hesabu ,kuzitamka kila siku kabla ya kulala na kila siku anapotendea na kufanya mazoezi ya kutosha ya somo la hisabati.Ulipowadia wakati wa kufanya mitihani ya kuingia chuo kikuu .
Jack Ma alipata alama 79 ,ambazo zilikuwa ni alama za kawaida kwa watu wengine lakini kwake ndio ilikuwa alama kubwa katika historia ya taaluma yake, na kufanikiwa kupata alama ya kujiunga cho cha , Hangzhou Teacher's Institute na kusoma shahada ya B.A. in English .
Baada ya kumaliza chuo, Jack Ma aliomba kazi Zaidi ya 30 ,na alikosa nafasi zote za kazi aliziomba .Siku moja kampuni ya KFC yenye hotel katika nchi tofauti duniani kote ilifungua, hotel katika mji aliozaliwa Jack Ma , Hangzhou, Zhejiang, China .
Watu 24 walienda kuomba nafasi za kazi , na walibahatika kupata watu 23 kazi katika mgahawa wa KFC na Jack Ma alikose nafasi yeye peke yake ila hakukata tamaa,sababu fikra zake zilikuwa na njaa ya kutimiza ndoto zake.
Baadaye aliamua kuwa lecturer wa somo la English na International Trade katika chuo cha Hangzhou Dianzi University .Mwaka 1994 Jack Ma alisikia neno Internet na mwaka 1995 aliamua kwenda nchini Marekani yeye na rafiki zake kujifunza Zaidi maswala ya Internet.
Siku waliofika nchini Marekani ,walipokuwa kwenye internet Jack Ma na rafiki zake pamoja na mke wake waliamua kutafuta neno ‘’Beer’’,kisha wakapata habari nyingi kuhusu ‘’Beer’’ kutoka nchi mbali mbali duniani ila kwa bahati mbaya China haikuwepo kwenye majibu hayo.
Kisha akajaribu kutafuta habari zozote kuhusu nchi yake ya China ,pia akashangaa kutokuona taarifa yeyote kuhusu China.Ndipo yeye na rafiki zake na mke wake wakaamua kutengeneza mtandao walio upa jina ‘’Ugly’’ uliohusu mambo mbali mbali kuhusu nchi ya china.
Jack Ma na rafiki zake walizindua mtandao wa ‘’Ugly’’ saa 9:40 AM na ilipofika mida ya saa 12:30 PM ,watu wengi kutoka China ,walianza kumuulizia yeye na hiyo kampuni yake kujua mambo mbali mbali hapo ndipo Jack Ma .alipojua kuwa Internet ni silaha maridhawa ya kufanya biashara na watu mbali mbali dunia bila mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
April 1995 ,Jack Ma ,na rafiki zake pamoja na mke wake ,waliomba mkopo wa USD 20,000/- na kufungua kampuni yao waliyoipa jina la "China Yellow Pages." Iliyojishughulisha na kutengeneza website za makampuni toka China.Ndani ya miaka mitatu ‘’China Yellow Pages." Ilitengeneza kiasi cha USD 800,000/-. Wakati walianza na mtaji wa USD 20,000/-
Alibaba Group ilivumbuliwa April 4, 1999, Hangzhou, China na kuanzia mwaka October 1999 na January 2000,Alibaba ilipata kiasi cha $25 million kutoka kwenye mradi wa uwekezaji wa kigeni .Mtandao wa www.forbes.com ,unaonyesha Jack Ma ana utajiri wa USD 23.8 Billion na kumfanya kuwa tajiri wa 23 katika orodha ya matajiri wa dunia.
Darasa:Kukata tamaa ni dhambi kubwa ,jifunze kujifunza kupitia kwa Jack Ma,usikubali mtu akuambie kuwa wewe huwezi au hauna vigezo katika harakati za kufanikisha ndoto zako #AdamJ.KForex
Live your life the way that you want to live it, don’t let other people live it for you…
No comments:
Post a Comment