Breaking

Showing posts with label launeyempire..... Show all posts
Showing posts with label launeyempire..... Show all posts
July 18, 2017

Jamani Mwenzenu Demu Wangu ni Mjeuri, Anakiburi na Mkaidi Sana Nimfanyeje?

Wana Udaku naombeni msaada kwa huyu mdada sijui ata nini nimfanyie anakiburi na mjeuri ajabu akiambiwa tofauti na alivyotegemea ananuna wenda ata asiongee ama kama tunaongea kwa simu anakata na hapokei simu, nikimwambia nitamwacha analia na kulalamika eti nimepata mtu mwingine na ndiyo maana nimeamua kumwachaa,,,, kiukweli mimi ni mwaminifu ila sasa anaifanya niamini msemo ambao mwalimu wangu aliniambia nikiwa form two kwamba kuwa na demu mmoja unatafuta uginjwa wa moyo....kiukweli namppenda san na ndiyo maana sijaribu ata kumchiti ila sasa natamani ata ajikoze mdada mwenye kuhitaji mume tuendelee maana sasa inatosha naumia kiukweli acheni masihara kwa mapenzi yanauma kuliko kuchapwa mboko sure....msaada ata kama kuna mdada ambaye yupo siriasi naomba aje tujenge mahusiano ya kweli mimi naweza kumilikiwa bila ata kusumbua love you wanajamiii mnanielimisha mengi sana!

July 15, 2017

Hiki Ndicho Kinachoitwa Kichaa Cha Mapenzi

Kabla mtu hajaoa au kuolewa , huamini kabisa kwamba, kabla hajafanya mapenzi au tendo la ndoa na mtu anayemwita mpenzi wake, bado hawezi kudai kwamba, huyo mtu ni mpenzi wake na kwajibika kwake kama mpenzi.

Vijana wengi huamini kwamba, baada ya kukutana kimwili, ndipo wanaweza kudai kwamba, hao ni wapenzi wao na kwamba kukutana kimwili, ndiyo mapenzi au kupenda kwenyewe.

Inapotokea wanapokutana huvutiwa na tendo la ndoa, huamini kabisa kwamba, uhusiano nao utakuwa mzuri. Kwao, tendo la ndoa ndio kipimo cha uimara wa uhusiano wao.

Baada ya kufanya mapenzi, wapenzi hao huamini kwamba, sasa wanaweza kujitolea kwenye uhusiano huo na kwamba, wanaweza kuwa na nguvu nao kwa asilimia kubwa.

Suala hili, kuna wataalamu huliita mtego wa kimapenzi. Huitwa hivyo, kwa sababu huwafanya wapenzi kutokuangalia sifa nyingine na badala yake kuweka nguvu kwenye mwili, yaani tendo la ndoa.

Upofu hutokea kutokana na kuzalishwa kwa kemikali nyigi mwilini, zenye kumfanya mtu asiweze kujiuliza kuhusu maeneo mengine ya kimasha ya binadamu, zaidi  ya mwili.

Kinachotokea ni mwili kuvutwa na wale tunaowapenda kwa kuzalisha homoni inayofahamika kama ‘phenylethylamine’ au PEA kwa kifupi.

Kemikali au homoni hii pamoja na nyingine kama vile ‘depomine’ na ‘norepinephrine’ (ambazo huchochea hali za kimwili) na ‘ testosterone’(ambayo huongeza hamu ya kujaamiana), huzalishwa mara baada ya kukutana kimwili.

Baada ya kuzaliswa kwa homoni hizi, akili ya mtu huona mwili tu, yaani mapenzi na siyo sifa nyingine. Hapa ndipo ambapo, mtu hujikuta hawezi kujizuia tena kukutana kimwili na mpenzi wake, mara baada ya kukutana naye mara ya moja.

Baada ya kufanya mapenzi na kufikia kileleni, huzalishwa homoni iitwayo ‘oxytocin’ (ambayo huhusika na mihemiko), homoni hii humfanya mtu kujikuta anapenda kuwa karibu na kujifungamanisha na mtu aliyefanya naye mapenzi. Tunaweza kusema, ukaribu kwa wapenzi wawili huongezeka na unakuwa ni ukaribu wa mwili zaidi.

Kuzalishwa kwa homoni hizi, ni jambo ambalo mtu hawezi kulizuia na huwa linakuja kwa nguvu sana, kiasi kwamba, mtu kuwa kama amepoteza ufahamu wa maeneo mengineyo ya kimaisha isipokuwa mapenzi tu.

Homoni hizi humfanya mtu kuwa na hisia za kuvutiwa na mwingine, uchangamfu, ukaribu, kuvutiwa na hisia za ukamilifu zaidi. Wale waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya ndoa au wale waliowahi au wanaotoka nje ya ndoa zao kwa kuvutwa kimwili na wapenzi wengine, wanajua inavyokuwa.

Lakini homoni hizi, hatimaye huanza kupungua na mtu huanza kuhisi kwamba alikosea. Huoni tena na huhisi kama ilivyokuwa awali. Sasa haoni kuwa mpenzi wake ni mzuri au anafaa kama iivyokuwa awali. Kwa sababu, homoni zile zimeshuka sana, mwili unakuwa hauna maana tena.

Kwa bahati mbaya  kile kilichokuwa kinaitwa upendo, kilikuwa kimefungiwa kwenye mwili na homoni hizo ambazo kwa sasa hazipo. Hivyo, wapenzi hawana kingine cha kushika ambacho, wataweza kukiita mapenzi.

Unajua sasa ni kwa nini, tangu kale kabisa suala la wachumba kukutana kimwili kabla ya ndoa lilikuwa likipingwa sana? ni kwamba, watu wanapokutana kimwili, uwezo wa kukaguana tabia unakuwa umefungwa kutokana na kufumuka kwa homoni hizi, ambazo hubadili hali ya mtu na hisia zake kwa ujumla.

Kwa nini unadhani watu, hasa wanaume wakishaanza mapenzi ya kimwili na mtu mpya, yaani nyumba ndogo au yeyote, inakuwa rahisi sana kwao kujisahau na kukamatwa? Sababu ni hiyo hiyo, kwamba, uzalishwaji wa homoni hizi huwa ni mkubwa kiasi cha mtu kuamini kwamba, hakuna kingine chene kufurahisha na kuliwaza kama uhusiano huo.

Kumbuka, watu wawili wanapovutana, kwa maneno mengine tunasema kuna kemia kati yao. Hii ina maana kwamba, huwa kuna mabadiliko ya badhi ya homoni kama nilivyosema. Lakini,

wanapokutana, homoni hizi huwa nyingi kiasi cha kufanya upofu wa muda. Unaweza kuwa upofu wa mwezi, mwaka au miaka.

Upofu huu unapmalizika, uhusianao huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema awali, hqakuna mahali pengine pa kushika  siyo tabia, mienenfo waa haiba.

Upofu huu unapomalizika, uhusiano huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema awali, hakuna mahali pengine pa kushika siyo tabia, mienendo wala haiba.

Inashauriwa kwamba, mtu anapovutiwa na mwingine au watu wanapovutana ni vema wakawa wangalifu sana. kwanza, wajue kwamba, uhusino ambao msingi wake ni miili tu, yaani tendo la ndoa haudumu, kwani homoni zitokanazo na kukutana watu kimwili, hazina maisha, huwa zinaisha haraka.

Lakini pia inashauriwa kwamba, mtu anapoingia kwenye mapenzi ajaribu kushariana au kuukagua moyo wake, akili pamoja na hisia zake. Kuacha tu mabadiliko ya hali ya mwili yakatawala ni kutafuta maumivu.

Hebu jiulize, ni kwa nini mapenzi yanapoanza kwa moto sana, huzimika haraka  au kwa kishindo sana? ni kwa sababu yanajengwa kwenye msingi usioaminika, yaani katika mihemiko na kimapenzi. Penzi linalokua polepole ndilo lenye kushika, kwani halina msingi wa mwili.

July 14, 2017

Hizi Ndizo Sababu za Lulu Kupungua

MSANII kutoka Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa mara ya kwanza amefungukia sababu zinazomfanya kupungua sana mwili kuwa ni kushinda kwa kula matunda pamoja na mazoezi makali ya viungo.
Akizungumza na Star Mix, Lulu alisema kuwa, ameamua kupunguza mwili kwa makusudi na kwamba kila siku anashinda akila matunda na kufanya mazoezi magumu ya viungo.
“Watashangaa sana kuniona napungua lakini nafanya hivi wala sijashauriwa na mtu ni kuweka tu mwili wangu sawa. Nafanya sana mazoezi, naenda gym kila siku na kuhakikisha muda mwingi nashinda kwa kula matunda kuliko chakula,” alisema Lulu.
Wiki mbili zilizopita, Lulu alizua gumzo katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar baada ya kuonekana akiwa amepungua tofauti na zamani.
July 14, 2017

Rufaa Vyeti Feki: 600 Wagonga Mwamba, 450 Warudishwa Kazini

Watumishi wa umma 450 walioondolewa kazini kutokana na kudaiwa kutumia vyeti vya kughushi wamerudishwa kazini baada ya kushinda rufaa zao.

Baada ya kutangazwa kwa Orodha ya watumishi wenye vyeti feki, 1050 walikata Rufaa huku  8800 wakiridhika na matokeo hayo.

Mbali na hilo, Serikali imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk.Laurean Ndumbalo alisema watumishi hao wameshinda rufaa zao hivyo wataandikiwa barua za kurudishwa katika utumishi wa umma.

Alisema katika rufaa hizo, wengi walikuwa wanawake walioolewa na kubadili majina yao kwa kutumia ya waume zao.

“Kuna baadhi walitumia majina mawili alipokuwa kidato cha nne baadaye alilazimika kutumia matatu na kusababisha mkanganyiko hivyo tumejiridhisha na wanarudishwa katika utumishi wa umma,” alisema Dk. Ndumbalo.

Alisema Serikali pia imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

“Serikali imesitisha mishahara ya watumishi wote ambao muundo wa utumishi wao uliwataka kuwa na sifa ya kufaulu kidato cha nne wakati wanaajiriwa lakini hawakuwasilisha vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani.

“Tunasitisha mishahara yao kuanzia mwezi Julai hadi hapo watakapowasilisha vyeti vyao kuhakikiwa,” alisema Dk. Ndumbalo.

Dk. Ndumbalo aliongeza kuwa kwa watumishi walioajiriwa wakiwa darasa la saba kabla ya waraka wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2004 uliowataka waajiriwa kuwa na sifa ya kidato cha nne, wataendelea na kazi mpaka watakapostaafu.

Alisema sera ya Menejimenti na Ajira katika utumishi wa umma toleo la mwaka 1998 lilianza kutekelezwa Mei 20, 2004 hivyo kwa walioajiriwa kabla ya hapo warudishwe kazini kama waliondolewa kimakosa.

“Nasisitiza kuwa watumishi wote wa umma walioajiriwa kwa sifa ya elimu ya darasa la saba kabla ya Mei 20 hawahusiki na uhakiki wa vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne na wataendelea kuwa watumishi wa umma katika vyeo vyao mpaka watakapostaafu kazi,” alisema Dk.Ndumbalo.

Aidha alisema serikali inatangaza ajira mpya 10,184 katika sekta mbalimbali huku ikitoa ajira 3,172 kwa sekta ya afya.

July 14, 2017

Kimenuka...Machangudoa Waundiwa Vikundi vya Ulinzi Moshi

 Wananchi wa Kata ya Mawenzi, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo.

Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio.

Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo, amesema tatizo la machangudoa kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo limekuwa kero nyakati za usiku pamoja na vijana wanaofanya uhalifu pia wamesababisha watu kuwa na hofu ya usalama wao.

Mkazi wa kata hiyo, Mary William, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo.

Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa jambo hilo.

“Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na  uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi.

Akijibu kero za wananchi hao kuhusu kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni.

Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael, amesema suala lao limeshapitishwa bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili.

Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.